Siachani Nawe by Baraka da Prince
- Mar 23, 2016
- 1 min read
(verse1) Wakati nalainisha moyo kupenda sio kama ninakosea ipo sababu ya mimi kurejesha namba ambayo ilipotea hali ya mtoto kumsusa mama akishachapwa ni sawa na mapenzi ukishapendwa unasahau hata kama ulishafanyiwaga ushenzi nakumbuka nilijuta sana kupenda kupenda kusikokua na thamani ila hitaji la moyo lalazimisha kurudia zamani
(chorus) mimi bado nina imani ipo siku utanipa thamani mimi bado nina imani jua me siachani nawe na sishindani nawe maana upo moyoni ndani acha nisote mie ila me siachani nawe na sishindani nawe maana upo moyoni ndani wacha nisote mie (verse2) labda juu ya kaburi utanipenda mimi nikiwa sina uhai hisia zangu haziheshimiwi najidharau sifai heri ya upofu wa macho kwa yale nayoyaona umeruhusu mboni zangu me kumwaga machozi yaani ungejua hisia za mapenzi kutesa moyo ila bado hazichoshi kupendwa sipendwi najua wazi ila bado silingi maana kesho nitaurubuni moyo unapendwa na unapenda me meno ila najiona kibogoyo kweli penzi donda moyo (chorus) mimi bado nina imani ipo siku utanipa thamani mimi bado nina imani jua me siachani nawe na sishindani nawe maana upo moyoni ndani acha nisote mie ila me siachani nawe na sishindani nawe maana upo moyoni ndani wacha nisote mie






Comments